A A A A A

Sünden: [Ehebruch]


1 Korinther 6:18
Flieht die Unzucht! Denn jede Sünde, die ein Mensch begeht, bleibt außerhalb des Leibes; der Unzüchtige dagegen sündigt an seinem eigenen Leibe.

2 Mose 20:14
Du sollst nicht ehebrechen!

Hebräer 13:4
Die Ehe sei bei allen ehrbar und unbefleckt das Ehebett. Unzüchtige und Ehebrecher wird Gott richten.

Jakobus 4:17
Wer aber Gutes zu tun weiß und es nicht tut, dem ist es Sünde.

Jeremia 13:27
Nimeona machukizo yako, naam, uzinifu wako, na ubembe wako, na uasherati wa ukahaba wako, juu ya milima katika mashamba. Ole wako, Ee Yerusalemu! Hutaki kutakaswa; mambo hayo yataendelea hata lini?

1 Johannes 1:9
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

Lukas 16:18
Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Matthäus 19:9
Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Sprüche 6:32
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Römer 7:2-3
[2] Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.[3] Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.

Markus 10:11-12
[11] Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;[12] na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.

Matthäus 5:27-32
[27] Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;[28] lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.[29] Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.[30] Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.[31] Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;[32] lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

1 Korinther 6:9-16
[9] Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,[10] wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.[11] Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.[12] Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.[13] Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.[14] Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.[15] Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha![16] Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

Lukas 18:18-20
[18] Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?[19] Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.[20] Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

1 Thessalonicher 4:3-5
[3] Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;[4] kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;[5] si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

Markus 7:20-23
[20] Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.[21] Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,[22] wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.[23] Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Matthäus 15:17-20
[17] Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?[18] Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.[19] Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;[20] hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.

Sprüche 5:18-23
[18] Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.[19] Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.[20] Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?[21] Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote huitafakari.[22] Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.[23] Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

Johannes 8:4-11
[4] Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.[5] Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?[6] Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.[7] Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.[8] Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.[9] Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.[10] Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?[11] Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Sprüche 6:20-35
[20] Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.[21] Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.[22] Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.[23] Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.[24] Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.[25] Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.[26] Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani[27] Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?[28] Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?[29] Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.[30] Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;[31] Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.[32] Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.[33] Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.[34] Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.[35] Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.

Sprüche 5:3-22
[3] Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;[4] Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.[5] Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;[6] Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.[7] Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu.[8] Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.[9] Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako;[10] Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;[11] Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;[12] Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;[13] Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha![14] Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.[15] Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.[16] Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?[17] Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.[18] Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.[19] Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.[20] Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?[21] Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote huitafakari.[22] Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.

1 Korinther 7:1-40
[1] Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.[2] Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.[3] Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.[4] Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.[5] Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.[6] Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.[7] Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.[8] Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.[9] Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.[10] Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;[11] lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.[12] Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.[13] Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.[14] Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.[15] Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.[16] Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?[17] Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.[18] Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.[19] Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.[20] Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa.[21] Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.[22] Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.[23] Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.[24] Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.[25] Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.[26] Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo.[27] Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke.[28] Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.[29] Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;[30] na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.[31] Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.[32] Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;[33] bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.[34] Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.[35] Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.[36] Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.[37] Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.[38] Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.[39] Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.[40] Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.

Swahili Bible 1997
1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved.