A A A A A


Tafuta

Matthayo 4:10
Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, nawe utamtumikia yeye peke yake.’ ”


Matthayo 12:26
Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama?


Matthayo 16:23
Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”


Marko 1:13
naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia.


Marko 3:23
Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani?


Marko 3:26
Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe akiwa amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia.


Marko 4:15
Hawa ndio wale walio kando ya njia, ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao.


Marko 8:33
Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, “Rudi nyuma yangu Shetani! Wewe huwazi yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu.”


Luka 10:18
Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme wa radi.


Luka 11:18
Kama Shetani amegawanyika mwenyewe ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli.


Luka 13:16
Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya Sabato?”


Luka 22:3
Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili.


Luka 22:31
Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano.


Yohane 13:27
Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. Yesu akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda litende haraka.”


Waroma 5:3
Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?


Waroma 10:38
Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.


Waroma 26:18
uyafumbue macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni na kutoka kwenye nguvu za Shetani, wamgeukie Mungu ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswa kwa kuniamini mimi.’


Matendo ya Mitume 16:20
Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. Amen.


1 Wakorinto 5:5
mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, ili roho yake iokolewe katika siku ya Bwana.


1 Wakorinto 7:5
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.


1 Wakorinto 10:20
La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani.


1 Wakorinto 10:21
Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.


2 Wakorinto 2:11
ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.


2 Corinthians 11:14
Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru.


2 Corinthians 11:15
Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.


2 Corinthians 12:7
Ili kunizuia nisijivune kwa sababu ya ufunuo huu mkuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese.


Waefeso 6:11
Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za Shetani.


1 Wathesalonike 2:18
Maana tulitaka kuja kwenu, hasa mimi Paulo, nilitaka kuja tena na tena, lakini Shetani akatuzuia.


2 Wathesalonike 2:9
Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo


1 Timotheo 1:20
Miongoni mwao wako Himenayo na Aleksanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.


1 Timotheo 3:6
Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya Shetani.


1 Timotheo 4:1
Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.


1 Timotheo 5:15
Kwa maana kwa kweli wajane wengine wamepotoka ili kumfuata Shetani.


Waebrania 2:14
Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani,


Yakobo 2:19
Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.


Yakobo 3:15
Hekima ya namna hiyo haishuki kutoka mbinguni bali ni ya kidunia, tabia ya kibinadamu wala si ya kiroho bali ni ya kishetani.


Yakobo 4:7
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.


Ufunuo wa Yohane 2:9
Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, wao ni sinagogi la Shetani.


Ufunuo wa Yohane 2:10
Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Ufunuo wa Yohane 2:13
Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambako ndiko anakokaa Shetani.


Ufunuo wa Yohane 2:24
Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo wengine wanayoyaita mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wo wote juu yenu):


Ufunuo wa Yohane 3:9
Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watatambua ya kwamba nimekupenda.


Ufunuo wa Yohane 9:20
Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea.


Ufunuo wa Yohane 12:9
Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.


Ufunuo wa Yohane 12:12
Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!”


Ufunuo wa Yohane 18:2
Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli uliye Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.


Ufunuo wa Yohane 20:2
Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ndiye ibilisi na Shetani, naye akamfunga kwa muda wa miaka 1,000.


Ufunuo wa Yohane 20:7
Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake,


Swahili Bible 2015 Contemporary
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission