A A A A A


Tafuta

Matthayo 1:18
Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Matthayo 1:20
Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Matthayo 3:11
“Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Matthayo 3:16
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikamfungukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake.


Matthayo 4:1
Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kuingia nyikani ili akajaribiwe na ibilisi.


Matthayo 5:3
“Heri walio maskini wa roho, maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.


Matthayo 10:20
Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.


Matthayo 10:28
Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali, mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu


Matthayo 12:18
“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho yangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa.


Matthayo 12:28
Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.


Matthayo 12:31
Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.


Matthayo 12:32
Mtu ye yote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini ye yote anenaye neno dhidi ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao.


Matthayo 22:37
Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’


Matthayo 22:43
Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa Roho, anamwita Kristo ‘Bwana’? Kwa maana asema,


Matthayo 26:41
Kesheni na muombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”


Matthayo 27:50
Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.


Matthayo 28:19
Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,


Marko 1:8
Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”


Marko 1:10
Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua.


Marko 1:12
Wakati huo huo, Roho akamwongoza Yesu kwenda nyikani,


Marko 3:29
Lakini ye yote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.”


Marko 12:30
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’


Marko 12:36
Kwa maana Daudi mwenyewe akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu alisema: “ ‘BWANA alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’


Marko 13:11
Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke kuhusu mtakalosema. Semeni tu lo lote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi msemao bali ni Roho Mtakatifu.


Marko 14:38
Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”


Marko 15:37
Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.


Marko 15:39
Basi yule jemadari, aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu, aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”


Luka 1:15
Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji cho chote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake.


Luka 1:17
Naye atatangulia mbele za Bwana katika roho na nguvu ya Eliya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki na kuliweka tayari taifa lililoandaliwa kwa ajili ya Bwana.”


Luka 1:35
Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu.


Luka 1:41
Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu,


Luka 1:47
nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu,


Luka 1:67
Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:


Luka 1:80
Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.


Luka 2:25
Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.


Luka 2:26
Roho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Kristo wa Bwana.


Luka 2:27
Simeoni akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria,


Luka 3:16
Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuliko mimi ambaye sistahili hata kufungua kamba ya viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Luka 3:22
Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua na sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa nawe sana.”


Luka 4:1
Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani,


Luka 4:14
Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.


Luka 4:18
“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwaletea maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa


Luka 8:55
Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara. Akaamuru apewe kitu cho chote cha kula.


Luka 10:21
Saa ile ile, Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu akasema, “Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na wenye akili, nawe umewafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hayo ndiyo yaliyokuwa mapenzi yako.


Luka 10:27
Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote, tena mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”


Luka 11:13
Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wale wamwombao!”


Luka 12:10
Naye kila atakaye nena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini ye yote atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.


Luka 12:12
Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.”


Луки 21:19
Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.


Луки 21:26
Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za vitu vya angani zitatikisika.


Луки 23:46
Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.


Waroma 1:2
hadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maelekezo kwa njia Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua.


Waroma 1:5
Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku hizi chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”


Waroma 1:8
Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”


Waroma 1:16
“Ndugu zangu, ilibidi maandiko yatimie yale ambayo Roho Mtakatifu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Yesu.


Waroma 2:4
Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.


Waroma 2:17
“ ‘Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto.


Waroma 2:18
Hata juu ya watumishi wangu nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.


Waroma 2:33
Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.


Waroma 2:38
Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Waroma 4:8
Petro akiwa amejaa Roho Mtakatifu akajibu, “Enyi watawala na wazee wa watu,


Waroma 4:25
Wewe ulisema kwa Roho Mtakatifu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: “ ‘Mbona watu Mataifa wanaghadhibika, na kabila za watu zinawaza ubatili?


Waroma 4:31
Walipokwisha kuomba, mahali pale walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.


Waroma 5:3
Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?


Waroma 5:9
Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho Mtakatifu wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.”


Waroma 5:32
Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.”


Waroma 6:3
Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii,


Waroma 6:5
Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho Mtakatifu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao mwongofu wa kutoka Antiokia.


Waroma 6:10
Lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala huyo Roho ambaye alisema kwake.


Waroma 7:51
“Ninyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zetu.


Waroma 7:55
Lakini yeye Stefano akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu.


Waroma 7:59
Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Yesu, pokea roho yangu”


Waroma 8:15
Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu,


Waroma 8:16
kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu.


Waroma 8:17
Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho Mtakatifu.


Waroma 8:18
Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, akawapa fedha


Waroma 8:19
akisema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apate kupokea Roho Mtakatifu.”


Waroma 8:29
Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”


Waroma 8:39
Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi.


Waroma 9:17
Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.”


Waroma 9:31
Ndipo kanisa katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria likafurahia wakati wa amani. Likatiwa nguvu na likaendelea kudumu katika kumcha Bwana na kwa faraja ya Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.


Waroma 10:19
Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta.


Waroma 10:38
Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.


Waroma 10:44
Wakati Petro akiwa anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe.


Waroma 10:45
Wale wa tohara walioamini waliokuwa wamekuja pamoja na Petro walishangaa kuona kuwa kipawa cha Roho Mtakatifu kimemwagwa juu ya watu Mataifa.


Waroma 10:47
“Je, kuna mtu ye yote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.”


Waroma 11:12
Roho Mtakatifu akaniambia niende nao bila kuwa na ubaguzi kati yao na sisi. Hawa ndugu sita pia walifuatana nami, nasi tukaingia nyumbani mwa huyo Kornelio.


Waroma 11:15
“Nami nilipoanza kusema, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama vile alivyotushukia sisi hapo mwanzo.


Waroma 11:16
Nami nikakumbuka neno la Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu.’


Waroma 11:24
Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana.


Waroma 11:28
Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.


Waroma 13:2
Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.”


Waroma 13:4
Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro.


Waroma 13:9
Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule Elima mchawi,


Waroma 13:52
Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.


Waroma 15:8
Mungu, yeye ajuaye mioyo, alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama vile alivyotupa sisi.


Waroma 15:28
Kwa maana imempendeza Roho Mtakatifu na sisi tusiwatwike mzigo wo wote mkubwa zaidi ya mambo haya yafuatayo ambayo ni ya lazima:


Waroma 16:6
Paulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Frigia na Galatia, wakiwa wamekatazwa na Roho Mtakatifu wasihubiri neno huko Asia.


Waroma 16:7
Walipofika kwenye mpaka wa Misia, wakajaribu kuingia Bithinia lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.


Waroma 18:25
Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Yesu, ingawa alijua tu ubatizo wa Yohana.


Waroma 19:2
akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.”


Waroma 19:6
Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri.


Waroma 19:21
Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.”


Waroma 20:22
“Nami sasa nimesukumwa na Roho, ninakwenda Yerusalemu wala sijui ni nini kitakachonipata huko.


Waroma 20:23
Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja.


Waroma 20:28
Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.


Waroma 21:4
Baada ya kuwatafuta wanafunzi wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale wanafunzi wakiongozwa na Roho wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu.


Waroma 21:11
Alipotufikia akachukua mshipi wa Paulo akajifunga, akautumia kufunga mikono na miguu yake mwenyewe akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwenye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu Mataifa.’ ”


Waroma 23:8
(Kwa maana Masadukayo wanasema kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho, lakini Mafarisayo wanaamini haya yote.)


Waroma 23:9
Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa sheria ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lo lote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”


Waroma 28:25
Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho Mtakatifu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu kwa kinywa cha Isaya kwamba:


Matendo ya Mitume 1:4
na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani, Yesu Kristo Bwana wetu.


Matendo ya Mitume 1:11
Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuweka juu yenu karama za rohoni ili mwe imara,


Matendo ya Mitume 2:29
Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani na tohara ya kweli ni jambo la rohoni, ni la kiroho, wala si la kimwili. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.


Matendo ya Mitume 5:5
wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.


Matendo ya Mitume 7:6
Lakini sasa, kwa kufia kile kilichokuwa kimetufunga kwanza, tumewekwa huru kutoka katika sheria ili tutumike katika njia mpya ya Roho, wala si katika njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.


Matendo ya Mitume 7:14
Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi.


Matendo ya Mitume 8:1
Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.


Matendo ya Mitume 8:2
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.


Matendo ya Mitume 8:4
ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.


Matendo ya Mitume 8:5
Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.


Matendo ya Mitume 8:6
Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani.


Matendo ya Mitume 8:9
Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.


Matendo ya Mitume 8:10
Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.


Matendo ya Mitume 8:11
Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.


Matendo ya Mitume 8:13
kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.


Matendo ya Mitume 8:14
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio watoto wa Mungu.


Matendo ya Mitume 8:15
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, “Abba, yaani, Baba,”


Matendo ya Mitume 8:16
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu.


Matendo ya Mitume 8:23
Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.


Matendo ya Mitume 8:26
Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu kusikoweza kutamkwa.


Matendo ya Mitume 8:27
Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu.


Matendo ya Mitume 9:1
Ninasema kweli katika Kristo, wala sisemi uongo, dhamiri yangu inanishuhudia katika Roho Mtakatifu.


Matendo ya Mitume 12:11
Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.


Matendo ya Mitume 14:17
Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.


Matendo ya Mitume 15:5
Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu,


Matendo ya Mitume 15:13
Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.


Matendo ya Mitume 15:16
ili kuwa mhudumu wa Kristo Yesu kwa watu Mataifa nikiwa na huduma ya kikuhani ya kutangaza Injili ya Mungu, ili watu Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.


Matendo ya Mitume 15:19
kwa nguvu za ishara na miujiza, kwa uweza wa Roho wa Mungu, hivyo kuanzia Yerusalemu hadi maeneo yote ya kandokando yake mpaka Iliriko, nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu.


Matendo ya Mitume 15:27
Imewapendeza kufanya hivyo, naam, kwani ni wadeni wao. Kwa maana ikiwa watu Mataifa wameshiriki baraka za rohoni za Wayahudi, wao ni wadeni wa Wayahudi, ili Wayahudi nao washiriki baraka zao za mambo ya mwilini.


Matendo ya Mitume 15:30
Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho Mtakatifu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu.


1 Wakorinto 1:7
Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


1 Wakorinto 2:4
Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu


1 Wakorinto 2:10
Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu.


1 Wakorinto 2:11
Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.


1 Wakorinto 2:12
Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho yule atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure.


1 Wakorinto 2:13
Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa wale watu wa kiroho.


1 Wakorinto 2:14
Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni.


1 Wakorinto 2:15
Mtu wa kiroho hutambua mambo yote, lakini yeye mwenyewe hatambuliwi na mtu ye yote.


1 Wakorinto 3:1
Ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwilini, kama watoto wachanga katika Kristo.


1 Wakorinto 3:16
Je, hamjui ya kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?


1 Wakorinto 4:21
Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?


1 Wakorinto 5:3
Hata kama siko pamoja nanyi katika mwili, niko nanyi katika roho. Nami nimekwisha kumhukumu mtu huyo aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwapo.


1 Wakorinto 5:4
Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Yesu nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho na uweza wa Bwana Yesu ukiwepo,


1 Wakorinto 5:5
mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, ili roho yake iokolewe katika siku ya Bwana.


1 Wakorinto 6:11
Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.


1 Wakorinto 6:17
Lakini mtu aliyeungwa na Bwana anakuwa roho moja naye.


1 Wakorinto 6:19
Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,


1 Wakorinto 6:20
kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu.


1 Wakorinto 7:34
pia kuna tofauti kati ya mwanamke aliyeolewa na msichana bikira. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili awe mtakatifu kimwili na kiroho, lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe.


1 Wakorinto 7:40
Lakini kwa uamuzi wangu, naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mungu.


1 Wakorinto 9:11
Je, ikiwa sisi tulipanda mbegu ya kiroho miongoni mwenu, Je, itakuwa ni jambo kubwa iwapo tutavuna vitu vya mwili kutoka kwenu?


1 Wakorinto 10:3
Wote walikula chakula kile cha roho,


1 Wakorinto 10:4
na wote wakanywa kile kinywaji cha roho, kwa maana walikunywa kutoka katika ule mwamba wa roho uliofuatana nao, nao ule mwamba ulikuwa Kristo.


1 Wakorinto 12:1
Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu.


1 Wakorinto 12:3
Kwa hiyo nataka mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.


1 Wakorinto 12:4
Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.


1 Wakorinto 12:7
Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.


1 Wakorinto 12:8
Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo.


1 Wakorinto 12:9
Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya.


1 Wakorinto 12:10
Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, kwa mwingine tafsiri za lugha.


1 Wakorinto 12:11
Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo mwenyewe.


1 Wakorinto 12:13
Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


1 Wakorinto 14:1
Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.


1 Wakorinto 14:2
Kwa maana mtu ye yote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu ye yote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa Roho.


1 Wakorinto 14:12
Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kulijenga kanisa.


1 Wakorinto 14:14
Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda.


1 Wakorinto 14:15
Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, lakini nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia.


1 Wakorinto 14:16
Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema?


1 Wakorinto 14:32
Roho za manabii huwatii manabii.


1 Wakorinto 14:37
Kama mtu ye yote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karama za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika ni maagizo kutoka kwa Bwana.


1 Wakorinto 15:44
unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia.


1 Wakorinto 15:45
Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima.


1 Wakorinto 15:46
Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho.


1 Wakorinto 16:18
Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa.


2 Wakorinto 1:22
kwa kututia muhuri wake na kutupa Roho wake mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia kile kijacho.


2 Wakorinto 3:3
Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.


2 Wakorinto 3:6
Yeye ndiye aliyetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.


2 Wakorinto 3:8
je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?


2 Wakorinto 3:17
Basi Bwana ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru.


2 Wakorinto 3:18
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.


2 Wakorinto 4:13
Imeandikwa, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Kwa roho yule yule wa imani pia tuliamini na hivyo tunasema,


2 Wakorinto 5:5
Basi Mungu ndiye aliyetufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo naye ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho.


2 Wakorinto 6:6
katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli,


2 Wakorinto 7:1
Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.


2 Wakorinto 7:13
Kwa ajili ya haya tumefarijika. Zaidi ya kule sisi kutiwa moyo, tulifurahi sana kumwona Tito alivyo na furaha, kwa sababu roho yake imeburudishwa na ninyi nyote.


2 Wakorinto 11:4
Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi.


2 Wakorinto 12:18
Nilimshawishi Tito aje kwenu, nami nilimtuma pamoja na ndugu yetu. Je, Tito aliwatumia ninyi ili kujipatia faida? Je, hatuenendi kwa Roho mmoja? Je, hatuchukui hatua zile zile?


2 Wakorinto 13:14
Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen.


Wagalatia 3:2
Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia?


Wagalatia 3:3
Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili?


Wagalatia 3:5
Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?


Wagalatia 3:14
Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.


Wagalatia 4:6
Kwa sababu ninyi ni watoto wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, anayelia, “Abba, Baba.”


Wagalatia 4:29
Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa.


Wagalatia 5:5
Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki.


Wagalatia 5:16
Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.


Wagalatia 5:17
Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, nayo Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.


Wagalatia 5:18
Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.


Wagalatia 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Wagalatia 5:25
Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.


Wagalatia 6:1
Ndugu zangu, ikiwa mtu ameghafilika akatenda dhambi, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejezeni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa.


Wagalatia 6:8
Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.


Wagalatia 6:18
Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikae pamoja na roho zenu. Amen.


Waefeso 1:3
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.


Waefeso 1:13
Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa,


Waefeso 1:17
Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.


Waefeso 2:2
ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii.


Waefeso 2:6
Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu,


Waefeso 2:18
Kwa maana kwa kupitia kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja.


Waefeso 2:22
Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya Roho wake.


Waefeso 3:5
Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu.


Waefeso 3:10
Ili sasa kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho,


Waefeso 3:16
Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,


Waefeso 4:3
Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani.


Waefeso 4:4
Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.


Waefeso 4:23
ili mfanywe upya roho na nia zenu,


Waefeso 4:30
Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.


Waefeso 5:18
Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.


Waefeso 5:19
Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu,


Waefeso 6:12
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Waefeso 6:17
Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.


Waefeso 6:18
Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.


Wafilipi 1:19
kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Yesu Kristo, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu.


Wafilipi 1:27
Lakini lo lote litakalotukia, mwenende kama ipasavyo Injili ya Kristo, ili kwamba nikija na kuwaona au ikiwa sipo, nipate kusikia haya juu yenu: Kuwa mnasimama imara katika roho moja, mkiishindania imani ya Injili kwa umoja,


Wafilipi 2:1
Kama kukiwa na jambo lo lote la kutia moyo, kukiwako faraja yo yote katika upendo, kukiwa na ushirika wo wote katika Roho, kukiwa na wema wo wote na huruma,


Wafilipi 2:2
basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia kama hiyo, mkiwa na upendo huo huo, wenye roho moja na kusudi moja.


Wafilipi 3:3
Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Kristo Yesu, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili,


Wafilipi 3:15
Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu ataliweka wazi hilo nalo.


Wafilipi 4:23
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.


Wakolosai 1:8
ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.


Wakolosai 1:9
Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatukukoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.


Wakolosai 2:5
Kwa maana ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi gani uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.


Wakolosai 3:16
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.


1 Wathesalonike 1:5
kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu.


1 Wathesalonike 1:6
Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu.


1 Wathesalonike 4:8
Kwa hiyo, mtu ye yote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.


1 Wathesalonike 5:19
Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu;


1 Wathesalonike 5:23
Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo.


2 Wathesalonike 2:2
msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.


2 Wathesalonike 2:13
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho kwa kuiamini kweli.


1 Timotheo 3:16
Bila shaka yo yote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.


1 Timotheo 4:1
Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.


2 Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.


2 Timotheo 1:14
Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.


2 Timotheo 4:22
Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.


Tito 3:5
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu,


Filemoni 1:25
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.


Waebrania 1:14
Je, malaika wote si roho watumikao waliotumwa kuwahudumia wale watakaorithi wokovu?


Waebrania 2:4
Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.


Waebrania 3:7
Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo: “Leo, kama mkiisikia sauti yake,


Waebrania 4:12
Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili, tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Waebrania 6:4
Kwa kuwa ni vigumu kuwarejeza tena katika toba wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu,


Waebrania 6:19
Tunalo tumaini hili lililo kama nanga ya roho, lililo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika patakatifu palipo nyuma ya pazia,


Waebrania 9:8
Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa anaonyesha kwamba maadamu ile hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakafifu ilikuwa bado haijafunguliwa.


Waebrania 9:14
Basi si zaidi sana damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa kutusafisha dhamiri zetu, kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai!


Waebrania 10:15
Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:


Waebrania 10:29
Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?


Waebrania 12:9
Tena, sisi sote tunao baba wa kimwili, waliotuadibisha nasi tukawaheshimu kwa ajili ya hilo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa Baba wa roho zetu ili tuishi?


Waebrania 12:23
kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mmekuja kwa Mungu, mhukumu wa watu wote, kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa,


Yakobo 2:26
Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.


Yakobo 3:15
Hekima ya namna hiyo haishuki kutoka mbinguni bali ni ya kidunia, tabia ya kibinadamu wala si ya kiroho bali ni ya kishetani.


Yakobo 4:5
Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa, huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?


Yakobo 5:20
hamna budi kujua kwamba ye yote amrejezaye mwenye dhambi kutoka katika upotovu wake, ataiokoa roho ya huyo mwenye dhambi kutoka katika mauti na kusitiri wingi wa dhambi.


1 Petro 1:2
Ninawaandikia ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo: Neema iwe nanyi na amani iongezwe kwenu.


1 Petro 1:9
Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.


1 Petro 1:11
wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.


1 Petro 1:12
Mitume walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali walihudumu kwa ajili yenu katika mambo hayo ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo ambayo hata malaika wanatamani kuyafahamu.


1 Petro 1:22
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.


1 Petro 2:2
Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine cho chote, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu,


1 Petro 2:5
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa kuwa nyumba ya Roho, mpate kuwa ukuhani mtakatifu, mkitoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.


1 Petro 2:11
Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu.


1 Petro 2:25
Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.


1 Petro 3:4
Badala yake kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa ndani, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu, ambako ni kwa thamani sana machoni pa Mungu.


1 Peter 3:18
Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho,


1 Peter 3:19
ambayo kwa hiyo alikwenda na kuzihubiria roho zilizokuwa kifungoni.


1 Peter 3:20
Roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Noa, wakati wa kujenga safina, ambako watu wachache tu, yaani, watu wanane waliokolewa wasiangamie kwa gharika.


1 Peter 4:6
Kwa kuwa hii ndiyo sababu Injili ilihubiriwa hata kwa wale waliokufa, ili kwamba wahukumiwe sawasawa na wanadamu wengine katika mwili, lakini katika roho waishi sawasawa na Mungu aishivyo.


1 Peter 4:14
Kama mkilaumiwa kwa ajili ya Jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu yenu.


1 Yohane 3:24
Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupatia.


1 Yohane 4:1
Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.


1 Yohane 4:2
Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu.


1 Yohane 4:3
Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.


1 Yohane 4:6
Sisi twatokana na Mungu na ye yote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.


1 Yohane 4:13
Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupatia sisi sehemu ya Roho wake.


1 Yohane 5:6
Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, yaani, Yesu Kristo. Hakuja kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.


1 Yohane 5:7
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni wamoja.


1 Yohane 5:8
Pia wako mashahidi watatu duniani], yaani Roho, Maji na Damu; wote hawa watatu wanakubaliana katika umoja.


3 Yohane 1:2
Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.


Yuda 1:19
Hawa ndio watu wanaowagawa ninyi, wafuatao tamaa zao za asili, wala hawana Roho.


Yuda 1:20
Lakini ninyi wapenzi, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu.


Ufunuo wa Yohane 1:4
Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja na kutoka kwa wale Roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi


Ufunuo wa Yohane 1:10
Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana, nikasikia sauti kubwa kama ya tarumbeta nyuma yangu


Ufunuo wa Yohane 2:7
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima, ambao uko katika paradiso ya Mungu.


Ufunuo wa Yohane 2:11
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa na mauti ya pili.


Ufunuo wa Yohane 2:17
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa yeye jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.


Ufunuo wa Yohane 2:29
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.


Ufunuo wa Yohane 3:1
“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Sardi andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.


Ufunuo wa Yohane 3:6
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.


Ufunuo wa Yohane 3:13
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.


Ufunuo wa Yohane 3:22
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.”


Ufunuo wa Yohane 4:2
Ghafula nilikuwa katika Roho, hapo mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu mmoja.


Ufunuo wa Yohane 4:5
Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu.


Ufunuo wa Yohane 5:6
Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote.


Ufunuo wa Yohane 6:9
Alipoivunja ile lakiri ya tano, nikaona chini ya madhabahu, roho za wale waliochinjwa kwa ajili ya Neno la Mungu na kwa ajili ya ushuhuda walioutunza.


Ufunuo wa Yohane 14:13
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”


Ufunuo wa Yohane 16:13
Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.


Ufunuo wa Yohane 16:14
Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.


Ufunuo wa Yohane 17:3
Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka nyikani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.


Ufunuo wa Yohane 18:13
mdalasini, vikolezi, uvumba, manemane, uvumba wenye harufu nzuri, divai, mafuta ya zeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, watumwa, pia na roho za wanadamu.


Ufunuo wa Yohane 18:14
“Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliyatamani yamekoma. Utajiri wako wote na fahari yako vimetoweka, wala haviwezi kupatikana tena kamwe!’


Ufunuo wa Yohane 19:10
Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”


Ufunuo wa Yohane 20:4
Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Nami nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudia huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000.


Ufunuo wa Yohane 21:10
Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, likishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.


Ufunuo wa Yohane 22:6
Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. BWANA, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”


Ufunuo wa Yohane 22:17
Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Ye yote mwenye kiu na aje na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure.


Swahili Bible 2015 Contemporary
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission