A A A A A


Tafuta

Luka 2:40
Naye mtoto Yesu akakua na kuongezeka nguvu akiwa amejaa hekima na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.


Luka 4:22
Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”


Yohane 1:14
Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Yohane 1:16
Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.


Yohane 1:17
Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.


Waroma 4:33
Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi na neema ya Mungu ilikuwa juu yao wote.


Waroma 6:8
Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu.


Waroma 11:23
Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote.


Waroma 13:43
Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu.


Waroma 14:3
Hivyo Paulo na Barnaba wakakaa huko kwa muda wa kutosha wakihubiri kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha ujumbe wa neema yake kwa kuwawezesha kufanya ishara na miujiza.


Waroma 14:26
Kutoka huko Atalia wakasafiri baharini kwa merikebu wakarudi mpaka Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile kazi waliokuwa wamekamilisha.


Waroma 15:11
Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu Kristo, kama wao wanavyookolewa.”


Waroma 15:40
Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana.


Waroma 18:27
Naye Apolo alipotaka kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika huko aliwasaidia sana wale watu ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini,


Waroma 20:24
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Yesu aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.


Waroma 20:32
“Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.


Matendo ya Mitume 1:5
Kwa kupitia kwake na kwa ajili ya Jina lake, tumepokea neema na utume ili kuwaita watu miongoni mwa watu wote wasiomjua Mungu, waje kwenye utii utokanao na imani.


Matendo ya Mitume 1:7
Kwa wote walioko Rumi wapendwao na Mungu na kuitwa kuwa watakatifu: Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.


Matendo ya Mitume 3:24
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.


Matendo ya Mitume 4:16
Kwa hiyo, ahadi huja kwa njia ya imani, ili iwe ni kwa neema na itolewe kwa wazao wa Abrahamu, si kwa wale walio wa sheria peke yao bali pia kwa wale walio wa imani ya Abrahamu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote.


Matendo ya Mitume 5:2
ambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu.


Matendo ya Mitume 5:15
Lakini ile karama iliyotolewa haikuwa kama lile kosa. Kwa maana ikiwa watu wengi walikufa kwa sababu ya kosa la mtu mmoja, zaidi sana neema ya Mungu na ile karama iliyokuja kwa neema ya mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo, imezidi kuwa nyingi kwa ajili ya wengi.


Matendo ya Mitume 5:16
Tena, ile karama ya Mungu si kama matokeo ya ile dhambi. Hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali karama ya neema ya Mungu ilikuja kwa njia ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.


Matendo ya Mitume 5:17
Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo.


Matendo ya Mitume 5:20
Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke. Lakini dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi.


Matendo ya Mitume 5:21
Ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu.


Matendo ya Mitume 6:1
Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka?


Matendo ya Mitume 6:14
Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.


Matendo ya Mitume 6:15
Ni nini basi? Je, tutende dhambi kwa kuwa hatuko chini ya sheria bali chini ya neema? La, hasha!


Matendo ya Mitume 11:5
Vivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu.


Matendo ya Mitume 11:6
Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.


Matendo ya Mitume 12:3
Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.


Matendo ya Mitume 12:6
Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani.


Matendo ya Mitume 15:15
Nimewaandikia kwa ujasiri vipengele kadha wa kadha katika waraka huu kama kuwakumbusha tena kwa habari ya ile neema Mungu aliyonipa,


Matendo ya Mitume 16:20
Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. Amen.


Matendo ya Mitume 16:24
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.


1 Wakorinto 1:3
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.


1 Wakorinto 1:4
Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu.


1 Wakorinto 3:10
Kwa neema Mungu aliyonipa, niliweka msingi kama mjenzi stadi na mtu mwingine anajenga juu ya huo msingi. Lakini kila mmoja inampasa awe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake.


1 Wakorinto 15:10
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.


1 Wakorinto 16:23
Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.


2 Wakorinto 1:2
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.


2 Wakorinto 1:12
Basi haya ndiyo majivuno yetu: Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeenenda katika ulimwengu na hasa katika uhusiano wetu na ninyi, katika utakatifu na uaminifu utokao kwa Mungu. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya kidunia bali kwa neema ya Mungu.


2 Wakorinto 4:15
Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.


2 Wakorinto 6:1
Kama watenda kazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.


2 Wakorinto 8:1
Basi sasa ndugu, nataka ninyi mjue kuhusu ile neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia.


2 Wakorinto 8:6
Kwa hiyo tulimsihi Tito, kwa kuwa ndiye aliyeanzisha jambo hili, akamilishe tendo hili la neema kwa upande wenu.


2 Wakorinto 8:7
Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.


2 Wakorinto 8:9
Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri.


2 Wakorinto 9:14
Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu.


2 Wakorinto 12:9
Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.


2 Wakorinto 13:14
Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen.


Wagalatia 1:3
Neema iwe nanyi na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


Wagalatia 1:6
Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata injili nyingine,


Wagalatia 1:15
Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake,


Wagalatia 2:9
Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, walioonekana kama nguzo za kanisa, walitupa mkono wa shirika, mimi na Barnaba walipotambua ile neema niliyopewa. Wakakubali kwamba sisi tuende kwa watu Mataifa na wao waende kwa Wayahudi.


Wagalatia 2:21
Siibatilishi neema ya Mungu, kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure!”


Wagalatia 3:18
Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi.


Wagalatia 5:4
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.


Wagalatia 6:18
Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikae pamoja na roho zenu. Amen.


Waefeso 1:2
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.


Waefeso 1:7
Katika yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake


Waefeso 2:5
hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema.


Waefeso 2:7
ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Kristo Yesu.


Waefeso 2:8
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu,


Waefeso 3:2
Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu,


Waefeso 3:7
Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.


Waefeso 3:8
Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na


Waefeso 4:7
Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.


Waefeso 6:24
Neema iwe na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wa dhati. Amen.


Wafilipi 1:2
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.


Wafilipi 1:7
Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu, ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami.


Wafilipi 4:23
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.


Wakolosai 1:2
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai: Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu.


Wakolosai 1:6
ile Injili iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote.


Wakolosai 4:6
Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.


Wakolosai 4:18
Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen.


1 Wathesalonike 1:1
Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo: Neema iwe kwenu na amani, itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.


1 Wathesalonike 5:28
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen.


2 Wathesalonike 1:2
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.


2 Wathesalonike 1:12
Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Yesu lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.


2 Wathesalonike 2:16
Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema,


2 Wathesalonike 3:18
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amen.


1 Timotheo 1:2
Kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani: Neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


1 Timotheo 1:14
Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.


1 Timotheo 6:21
ambayo wengine kwa kujidai kuwa nayo wameiacha imani. Neema iwe nanyi. Amen.


2 Timotheo 1:2
Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa: Neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


2 Timotheo 1:9
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya kuwako kwa ulimwengu.


2 Timotheo 2:1
Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu.


2 Timotheo 4:22
Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.


Tito 1:4
Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote: Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.


Tito 2:11
Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa.


Tito 3:7
ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi tukiwa na tumaini la uzima wa milele.


Tito 3:15
Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu wale wanaotupenda katika imani. Neema iwe nanyi nyote. Amen.


Filemoni 1:3
Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.


Filemoni 1:25
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.


Waebrania 2:9
Lakini twamwona Yesu, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.


Waebrania 4:16
Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


Waebrania 10:29
Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?


Waebrania 12:15
Angalieni sana mtu ye yote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.


Waebrania 13:9
Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria.


Waebrania 13:25
Neema iwe nanyi nyote. Amen.


Jakobus 4:6
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”


2 Petro 1:2
Neema na amani iwe kwenu kwa wingi katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.


2 Petro 3:18
Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.


2 Yohane 1:3
Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwanawe Baba, itakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.


Yuda 1:4
Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wapotoshao neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi wakimkana yeye aliye Bwana wetu wa pekee, Bwana Yesu Kristo.


Ufunuo wa Yohane 1:4
Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja na kutoka kwa wale Roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi


Ufunuo wa Yohane 22:21
Neema ya Bwana Yesu iwe na watakatifu wote. Amen.


Swahili Bible 2015 Contemporary
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission