A A A A A


Tafuta

Matthayo 5:8
Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.


Matthayo 5:28
Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.


Matthayo 6:21
Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa.


Matthayo 9:2
Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda. Yesu alipoona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu, dhambi zako zimesamehewa.”


Matthayo 9:21
kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”


Matthayo 9:22
Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.


Matthayo 11:29
Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu.


Matthayo 12:34
Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake.


Matthayo 12:40
Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, mchana na usiku.


Matthayo 13:19
Mtu ye yote anaposikia neno la Ufalme, naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake, hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia.


Matthayo 14:27
Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni Mimi. Msiogope.”


Matthayo 15:18
Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi.


Matthayo 15:19
Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.


Matthayo 16:23
Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”


Matthayo 18:35
“Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe kutoka moyoni kila mmoja ndugu yake aliyemkosea.”


Matthayo 22:37
Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’


Matthayo 24:48
Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’


Matthayo 26:38
Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.”


Marko 5:28
kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitapona.”


Marko 6:50
kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni Mimi, msiogope!”


Marko 7:19
Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Yesu alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”)


Marko 7:21
Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka: Mawazo mabaya, uasherati,


Marko 8:12
Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin, nawaambieni, hakitapewa ishara yo yote.”


Marko 10:49
Yesu akasimama na kusema, “Mwiteni.” Hivyo wakamwita yule mtu kipofu wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”


Marko 11:23
Amin, amin nawaambia, mtu ye yote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng'oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.


Marko 12:30
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’


Marko 12:33
Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa na dhabihu.”


Marko 14:34
Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.”


Marko 14:72
Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alilokuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.


Luka 1:29
Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?”


Luka 1:46
Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,


Luka 2:19
Lakini Maria akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari.


Luka 2:35
ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike na upanga utauchoma moyo wako.”


Luka 2:51
Ndipo akashuka pamoja nao hadi Nazareti, naye alikuwa mtii kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote.


Luka 6:45
Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo mabaya kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.


Luka 7:13
Bwana Yesu alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”


Luka 7:39
Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”


Luka 8:15
Lakini zile mbegu kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu na wa utii, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda.


Luka 10:27
Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote, tena mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”


Luka 12:17
Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’


Luka 12:34
Kwa maana hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwa pia.


Luka 12:45
Lakini ikiwa yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike na kula na kunywa na kulewa,


Luka 15:17
“Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!


Luka 15:20
Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.


Luka 16:3
“Yule msimamizi akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu ananiondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, nami ninaona aibu kuombaomba.


Luka 18:4
“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu,


Yohane 2:25
Hakuhitaji ushuhuda wa mtu ye yote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu.


Yohane 11:33
Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.


Yohane 13:2
Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu.


Yohane 13:21
Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”


Yohane 16:33
Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”


Waroma 1:24
Kisha wakaomba, wakasema, “Bwana, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua


Waroma 2:26
Kwa hiyo moyo wangu unafurahia na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utaishi kwa tumaini.


Waroma 2:46
Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe,


Waroma 4:32
Wale walioamini wote walikuwa na moyo mmoja na nia moja. Wala hakuna hata mmoja aliyesema cho chote alichokuwa nacho ni mali yake mwenyewe, lakini walishirikiana kila kitu walichokuwa nacho.


Waroma 5:3
Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?


Waroma 5:4
Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”


Waroma 8:21
Wewe huna sehemu wala fungu katika huduma hii kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.


Waroma 8:22
Kwa hiyo tubia huu uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini, aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.


Waroma 8:37
Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu).”


Waroma 11:23
Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote.


Waroma 13:22
Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Ambaye pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’


Waroma 14:22
wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.”


Waroma 15:31
Nao hao watu wakiisha kuisoma, wakafurahishwa sana kwa ujumbe wake wa kutia moyo.


Waroma 15:32
Yuda na Sila, ambao wenyewe walikuwa manabii wakanena maneno mengi ya kuwatia moyo na kuwajenga katika imani wale ndugu walioamini.


Waroma 16:14
Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanya biashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo.


Waroma 16:40
Baada ya Paulo na Sila kutoka gerezani walikwenda nyumbani kwa Lidia, ambapo walikutana na wale ndugu walioamini, wakawatia moyo, ndipo wakaondoka.


Waroma 17:16
Wakati Paulo akiwasubiri huko Athene, alisumbuka sana moyoni mwake kuona kwamba mji umejaa sanamu.


Waroma 18:27
Naye Apolo alipotaka kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika huko aliwasaidia sana wale watu ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini,


Waroma 20:1
Baada ya kumalizika kwa zile ghasia, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia.


Waroma 20:2
Alipopita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo, ndipo hatimaye akawasili Uyunani,


Waroma 21:13
Lakini Paulo akajibu, “Kwa nini mnalia na kunivunja moyo? Mimi niko tayari si kufungwa tu, bali hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.”


Waroma 23:11
Usiku uliofuata, Bwana akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama vile ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kunishuhudia huko Rumi pia.”


Waroma 27:22
Sasa ninawasihi sana, jipeni moyo mkuu kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake, ila meli itaangamia.


Waroma 27:25
Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia.’


Waroma 27:36
Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula.


Waroma 28:15
Ndugu wa huko Rumi waliposikia habari zetu, walikuja mpaka Soko la Apio na mahali paitwapo Mikahawa Mitatu kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akatiwa moyo.


Matendo ya Mitume 1:9
Kwa maana Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri Injili ya Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka


Matendo ya Mitume 1:12
au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi.


Matendo ya Mitume 5:4
nayo saburi huleta uthabiti wa moyo na uthabiti wa moyo huleta tumaini,


Matendo ya Mitume 6:17
Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa,


Matendo ya Mitume 9:2
Nina huzuni kuu na uchungu usiokoma moyoni mwangu.


Matendo ya Mitume 10:1
Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli, kwamba waokolewe.


Matendo ya Mitume 10:6
Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’ ” (yaani ili kumleta Kristo chini)


Matendo ya Mitume 10:8
Lakini andiko lasemaje? “Lile neno li karibu nawe, li kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, ni lile neno la imani tunalolihubiri.


Matendo ya Mitume 10:9
Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.


Matendo ya Mitume 10:10
Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.


Matendo ya Mitume 12:8
kama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.


Matendo ya Mitume 15:6
ili kwa moyo mmoja mpate kumtukuza Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.


1 Wakorinto 2:9
Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni, lile ambalo Mungu aliwaandalia wale wampendao”:


1 Wakorinto 5:8
Kwa hiyo, tusiiadhimishe sikukuu hii, kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, ndio weupe wa moyo na kweli.


1 Wakorinto 7:37
Lakini kama mwanaume ambaye ameshaamua moyoni mwake kutokuoa bila kulazimishwa na mtu ye yote, kama anaweza kujitawala kabisa; basi anafanya vyema kutokumwoa huyo mwanamwali.


1 Wakorinto 8:10
Kwa maana kama mtu ye yote mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi huu mkila katika hekalu la sanamu, je, si atatiwa moyo kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu?


1 Wakorinto 14:3
Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji.


1 Wakorinto 14:25
nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!”


1 Wakorinto 14:31
Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo.


2 Wakorinto 2:1
Hivyo nilikusudia moyoni mwangu nisifanye ziara nyingine yenye kuwaumiza ninyi.


2 Wakorinto 2:4
Kwa maana niliwaandikia kutokana na dhiki kubwa na kutaabika sana kwa moyo wangu tena kwa machozi mengi, shabaha yangu si ili niwasababishe mhuzunike bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.


2 Wakorinto 5:12
Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni.


2 Wakorinto 7:13
Kwa ajili ya haya tumefarijika. Zaidi ya kule sisi kutiwa moyo, tulifurahi sana kumwona Tito alivyo na furaha, kwa sababu roho yake imeburudishwa na ninyi nyote.


2 Wakorinto 8:16
Ninamshukuru Mungu ambaye amemtia Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali.


2 Wakorinto 9:7
Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.


Waefeso 6:5
Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo.


Waefeso 6:6
Watiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo.


Waefeso 6:7
Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu.


Waefeso 6:22
Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali zetu, na awatie moyo.


Wafilipi 1:7
Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu, ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami.


Wafilipi 1:14
Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.


Wafilipi 1:16
Hawa wa mwisho wanamhubiri Kristo kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba nimo humu gerezani kwa ajili ya kuitetea Injili.


Wafilipi 1:17
Hao wa kwanza wanamtangaza Kristo kutokana na tamaa zao wenyewe wala si kwa moyo mweupe bali wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu.


Wafilipi 2:1
Kama kukiwa na jambo lo lote la kutia moyo, kukiwako faraja yo yote katika upendo, kukiwa na ushirika wo wote katika Roho, kukiwa na wema wo wote na huruma,


Wafilipi 2:19
Natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu.


Wakolosai 2:2
Kusudi langu ni kuwa watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu kikamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe,


Wakolosai 3:12
Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu, wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.


Wakolosai 3:23
Lo lote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na si wanadamu.


Wakolosai 4:8
Nimemtuma kwenu kwa madhumuni haya ili kwamba mpate kufahamu hali yetu na pia awatie moyo.


1 Wathesalonike 2:12
Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza kuishi maisha yampendezayo Mungu, anayewaita katika Ufalme na utukufu wake.


1 Wathesalonike 2:17
Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa kitambo kidogo (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso.


1 Wathesalonike 3:2
tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi mwenzetu wa Mungu katika kuieneza Injili ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo katika imani yenu,


1 Wathesalonike 5:14
Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni wale wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na iweni na uvumilivu na kila mtu.


1 Timotheo 1:5
Kusudi la maagizo haya ni upendo, utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli.


2 Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.


2 Timotheo 2:22
Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.


Filemoni 1:7
Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.


Filemoni 1:12
Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa.


Filemoni 1:20
Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, uuburudishe moyo wangu katika Kristo.


Waebrania 3:12
Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.


Waebrania 3:13
Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.


Waebrania 4:12
Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili, tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Waebrania 6:18
Mungu alifanya hivyo, ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwa hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia, tuwe na moyo mkuu kulishika lile tumaini lililowekwa mbele yetu.


Waebrania 10:22
sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.


Yakobo 1:26
Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu.


1 Petro 1:22
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.


1 Petro 5:12
Kwa msaada wa Silvano, yeye ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.


1 Yohane 5:10
Kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu anao huu ushuhuda moyoni mwake. Kila mtu asiyemwamini Mungu amemfanya yeye kuwa mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda Mungu alioutoa kuhusu Mwanawe.


Ufunuo wa Yohane 1:3
Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na pia wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.


Ufunuo wa Yohane 18:7
Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’


Swahili Bible 2015 Contemporary
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission