A A A A A


Tafuta

Matthayo 2:3
Mfalme Herode aliposikia jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu.


मत्ती ९:८
Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama hii kwa wanadamu.


मत्ती १४:२६
Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.


मत्ती १४:३०
Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”


मत्ती १७:६
Wale wanafunzi, waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu.


मत्ती २८:८
Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini, wakiwa wamejawa na hofu lakini wenye furaha nyingi, wakaenda mbio ili kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo.


Luka 1:12
Zekaria alipomwona huyo malaika, akafadhaika sana akajawa na hofu.


Luka 1:65
Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote.


Luka 1:74
kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia yeye pasipo hofu


Luka 2:9
Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawang'aria kotekote, wakaingiwa na hofu.


Luka 5:26
Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.”


Luka 7:16
Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu, Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”


Luka 8:37
Ndipo watu wote wa nchi ile ya Wagerasi wakamwomba Yesu aondoke kwao, kwa sababu walikuwa wamejawa na hofu. Basi akaingia katika mashua akaondoka zake.


Luka 21:26
Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za vitu vya angani zitatikisika.


Luka 24:5
Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu?


Waroma 2:43
Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume.


Waroma 5:5
Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia.


Waroma 5:11
Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya.


Waroma 7:32
‘Mimi ndimi Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo.’ Mose alitetemeka kwa hofu na hakuthubutu kutazama.


Waroma 10:4
Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Waroma 19:17
Habari hii ikajulikana kwa Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la Bwana Yesu likaheshimiwa sana.


Waroma 22:29
Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi kwa minyororo.


Waroma 23:10
Ugomvi ukawa mkubwa kiasi kwamba yule jemadari akahofu kuwa wangemrarua Paulo vipande vipande, akaamuru vikosi vya askari vishuke na kumwondoa Paulo katikati yao kwa nguvu na kumleta ndani ya ngome ya jeshi.


Waroma 24:25
Naye Paulo alipokuwa akinena juu ya haki, kuwa na kiasi na juu ya hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu na kusema, “Hiyo yatosha sasa! Waweza kuondoka. Nitakapokuwa na wasaa nitakuita.”


Matendo ya Mitume 3:18
“Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.”


Matendo ya Mitume 8:15
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, “Abba, yaani, Baba,”


Matendo ya Mitume 13:7
Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.


1 Wakorinto 2:3
Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana.


1 Wakorinto 16:10
Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, mkaribisheni. Hakikisheni kwamba hana hofu yo yote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo.


2 Wakorinto 7:5
Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na raha. Tulisumbuliwa kila upande, kwa nje kulikuwa na mapigano na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu.


2 Wakorinto 7:11
Tazameni jinsi huzuni hii ya kimungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmethibitisha kuwa hamna hatia katika jambo hilo.


2 Wakorinto 7:15
Upendo wake kwenu unaongezeka sana anapokumbuka jinsi mlivyokuwa watii na kumpokea kwa hofu na kutetemeka.


2 Wakorinto 11:3
Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo.


2 Wakorinto 12:20
Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.


2 Wakorinto 12:21
Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi huko nyuma na wala hawajatubia uchafu wao, yaani, uasherati na ufisadi walioufanya.


Wagalatia 4:11
Nina hofu juu yenu, kwamba kazi niliyofanya kwa ajili yenu inaweza kuwa nimejitaabisha bure.


Waebrania 10:27
Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao utakaowaangamiza adui za Mungu.


Waebrania 12:21
Waliyoyaona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.”


1 Petro 1:17
Nanyi kama mnamwita Baba yeye ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.


1 Yohane 4:18
Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.


Yuda 1:12
Watu hawa ni dosari katika karamu zenu za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu, wakijilisha pasipo hofu. Wao ni mawingu yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo, miti isiyo na matunda wakati wa mapukutiko, ambayo hunyauka, iliyokufa mara mbili na kung'olewa kabisa.


Yuda 1:23
wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka kwenye moto; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.


Ufunuo wa Yohane 10:8
Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”


Ufunuo wa Yohane 11:11
Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.


Ufunuo wa Yohane 18:10
Watasimama mbali na kulia kwa hofu kutokana na mateso yake na kusema: “ ‘Ole! Ole Ee mji mkubwa, Ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’


Ufunuo wa Yohane 18:15
Wale wafanyabiashara waliotajirika kwa bidhaa hizo kutoka kwake watasimama mbali naye kwa hofu ya mateso yanayompata. Watalia na kuomboleza wakipiga kelele wakisema:


Swahili Bible 2015 Contemporary
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission