Instagram
English
A A A A A
Tafuta
أعمال ١٣:٢٦
Ndugu zangu, wana katika familia ya Ibrahimu na ninyi watu wengine ambao pia mnamwabudu Mungu wa kweli, sikilizeni! Habari kuhusu wokovu huu imeletwa kwetu.


أعمال ١٣:٤٧
Hivi ndivyo Bwana alivyotuambia kufanya: ‘Nimewafanya ninyi mwanga kwa ajili ya mataifa mengine, kuwaonesha watu ulimwenguni kote njia ya wokovu.’”


أعمال ٢٨:٢٨
Ninataka ninyi Wayahudi mjue kuwa Mungu ameupeleka wokovu wake kwa watu wasio Wayahudi. Watasikia!”


2 Wakorinto 1:6
Ikiwa tuko katika mateso, tuko kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na ikiwa tunafarijika, ni kwa sababu tuweze kuwafariji ninyi. Hili huwasaidia katika kuyakubali mateso yale yale tunayopata kwa uvumilivu.


2 Wakorinto 6:2
Mungu anasema, “Nilikusikia kwa wakati sahihi, na nikakusaidia siku ya wokovu.” Ninawaambia kwamba “wakati uliokubalika” ni huu sasa. Na “Siku ya wokovu” ni leo.


2 Wakorinto 7:10
Aina ya huzuni ambayo Mungu anaitaka inawafanya watu waamue kubadili maisha yao. Hili linawaelekeza kwenye wokovu, nasi hatuwezi kulijutia hilo. Lakini huzuni dunia huleta mauti.


Waefeso 6:17
Upokeeni wokovu wa Mungu kama chapeo yenu. Na chukueni upanga wa Roho, yaani mafundisho ya Mungu.


Wafilipi 1:28
Na hamtawaogopa wale walio kinyume nanyi. Imani yenu thabiti itakuwa kama ishara kwao ya kuangamia kwenu. Lakini kwa hakika ni ishara ya wokovu wenu. Na hiki ni kipawa kutoka kwa Mungu.


Wafilipi 2:12
Rafiki zangu wapendwa, daima mnatii yale mliyofundishwa. Kama mlivyotii nilipokuwa pamoja nanyi, ni muhimu zaidi na zaidi kwamba mtii wakati huu ambapo sipo pamoja nanyi. Hivyo ni lazima mwendelee kuishi katika namna inayoleta maana kwa wokovu wenu. Fanyeni hivi kwa wingi wa heshima na utii kwa Mungu.


2 Wathesalonike 2:14
Mungu aliwaita ninyi mpate wokovu. Aliwaita kwa kutumia Habari Njema tuliwahubiri. Mliitwa ili mshiriki katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.


2 Timotheo 2:10
Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili na wao waweze kuufikia wokovu unaopatikana katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.


2 Timotheo 3:15
Na unajua kwamba umeyajua Maandiko Matakatifu tangu ukiwa mtoto. Maandiko hayo yana uwezo wa kukupa hekima. Hekima hiyo itakuongoza hadi kwenye wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.


Waebrania 1:14
Malaika wote ni roho ambao humtumikia Mungu nao hutumwa kuwasaidia wale watakaoupokea wokovu.


Waebrania 2:3
Hivyo kwa hakika hata nasi tutaadhibiwa kama hatutauzingatia wokovu mkuu tulionao. Alikuwa ni Bwana Yesu aliyewaambia watu kwa mara ya kwanza juu ya wokovu huo. Na wale waliomsikiliza walithibitisha kwetu kuwa yale mambo yalikuwa ni kweli.


Waebrania 2:10
Mungu aliyeumba vitu vyote na ambaye kwa utukufu wake vitu vyote vipo; alitaka watu wengi wawe watoto wake na kuushiriki utukufu wake. Hivyo alifanya yale aliyohitaji kuyafanya. Alimkamilisha yeye anayewaongoza watu hao kuuelekea wokovu. Kwa njia ya mateso yake Mungu alimfanya Yesu kuwa Mwokozi mkamilifu.


Waebrania 6:9
Rafiki zangu, sisemi haya kwa sababu nafikiri kuwa yanawatokea ninyi. Kwa hakika tunatarajia kuwa mtafanya vizuri zaidi; kwamba mtayafanya mambo mema yatakayotokea katika wokovu wenu.


Waebrania 9:28
Hivyo Kristo alitolewa kama sadaka mara moja kuchukua dhambi za watu wengi. Na atakuja mara ya pili, lakini siyo kujitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi. Atakuja mara ya pili kuleta wokovu kwa wale wanaomngojea.


Yakobo 1:21
Hivyo acheni matendo yote machafu na kila uovu uliokaa karibu yenu, na mpokee kwa unyenyekevu mafundisho yaliyopandwa ndani ya mioyo yenu. Neno hilo, lina uwezo wa kuleta wokovu wa roho zenu.


1 Petro 1:5
Ni kwa ajili yenu ninyi ambao kwa njia ya imani, mnalindwa na nguvu za Mungu ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


1 Petro 1:9
Mnaupokea wokovu wenu ambao ni lengo la imani yenu.


1 Petro 1:10
Manabii waliotabiri juu ya neema ambayo ingeoneshwa kwenu, walipeleleza kwa makini na kwa uangalifu wakaulizia habari za wokovu huu.


Yuda 1:3
Rafiki wapendwa, nilitaka sana kuwaandikia kuhusu wokovu tunaoshiriki pamoja. Lakini nimejisikia kuwa ni muhimu niwaandikie kuhusu kitu kingine: Ninataka kuwatia moyo kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu aliwapa watakatifu wake. Mungu alitoa imani hii mara moja na ni nzuri wakati wote.


Ketab El Hayat (NAV) 1988
Holy Bible, New Arabic Version (Ketab El Hayat) Copyright © 1988, 1997 by Biblica, Inc.® All rights reserved worldwide.