A A A A A


Tafuta

Luka 1:28
Malaika alimwendea na kusema “Salamu! Bwana yu pamoja nawe; Kwa kuwa neema yake iko juu yako.”


Luka 1:30
Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu, kwa kuwa neema ya Mungu iko juu yako.


Yohane 1:16
Alikuwa amejaa neema na kweli ya Mungu, tulipokea kutoka baraka moja baada ya nyingine kutoka kwake.


Yohane 1:17
Hiyo ni kusema kuwa, sheria ililetwa kwetu kupitia Musa. Lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.


Waroma 13:43
Baada ya mkutano, watu wengi, Wayahudi na wale waliobadili dini zao na kufuata dini ya Kiyahudi, waliwafuata Paulo na Barnaba; nao waliwatia moyo watu hawa waendelee kuitumaini neema ya Mungu.


Waroma 14:3
Hivyo Paulo na Barnaba walikaa Ikonia kwa muda mrefu, na walihubiri kwa ujasiri kwa ajili ya Bwana. Waliwahubiri watu kuhusu neema ya Mungu. Bwana alithibitisha kwamba kile walichosema ni kweli kwa ishara na maajabu yaliyofanyika kufanyika kupitia wao.


Waroma 15:11
Hapana, tunaamini kuwa sisi na watu hawa tutaokolewa kwa namna moja iliyo sawa, ni kwa neema ya Bwana Yesu.”


Waroma 18:27
Apolo alitaka kwenda Akaya. Hivyo waamini wa Efeso wakamsaidia. Waliwaandikia barua wafuasi wa Bwana waliokuwa Akaya wakiwaomba wampokee Apolo. Alipofika pale, alikuwa msaada mkubwa kwa wale waliomwamini Yesu kwa sababu ya neema ya Mungu.


Waroma 20:24
Siujali uhai wangu mwenyewe. Jambo la muhimu zaidi ni mimi kuimaliza kazi yangu. Ninataka niimalize huduma ambayo Bwana Yesu alinipa niifanye, nayo ni kuwahubiri watu Habari Njema kuhusu neema ya Mungu.


Waroma 20:32
Sasa ninawaweka katika uangalizi wa Mungu. Ninategemea ujumbe wa neema yake kuwaimarisha ninyi. Ujumbe huo unaweza kuwapa ninyi baraka ambazo Mungu huwapa watakatifu wake wote.


Matendo ya Mitume 1:7
Waraka huu ni kwa ajili yenu ninyi nyote mlio huko Rumi. Kwani Mungu anawapenda na amewachagua kuwa watu wake watakatifu. Ninamwomba Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo, wawape ninyi neema na amani.


Matendo ya Mitume 3:24
Mungu ameamuru sisi sote tufunguliwe kutoka dhambini. Zawadi hii ya neema yake imekuja kwetu kupitia kile ambacho Kristo Yesu alikifanya ili tuwe huru.


Matendo ya Mitume 5:2
Kupitia imani yetu, Kristo ametufungulia mlango kuingia katika neema ya Mungu, tunayoifurahia sasa. Na tunashangilia sana kwa sababu ya tumaini tulilonalo la kushiriki utukufu wa Mungu.


Matendo ya Mitume 5:15
Lakini kipawa cha Mungu hakifanani na dhambi ya Adamu. Watu wengi walikufa kwa sababu ya dhambi ya mtu huyo mmoja. Lakini neema waliyopokea watu kutoka kwa Mungu ilikuwa kuu zaidi. Wengi walikipokea kipawa cha Mungu cha uzima kwa neema ya huyu mtu mwingine, Yesu Kristo.


Matendo ya Mitume 5:17
Mtu mmoja alitenda dhambi, hivyo kifo kikawatawala watu wote kwa sababu ya huyo mtu mmoja. Lakini sasa watu wengi wanaipokea neema ya Mungu iliyo nyingi sana na karama yake ya ajabu ya kufanyika wenye haki. Hakika watakuwa na uzima wa kweli na kutawala kupitia mtu mmoja, Yesu Kristo.


Matendo ya Mitume 5:20
Baada ya sheria kuja, zilikuwepo njia nyingi za watu kufanya makosa. Lakini kadri watu walivyozidi kufanya dhambi, ndivyo Mungu alivyomimina zaidi neema yake.


Matendo ya Mitume 5:21
Hapo kale dhambi ilitumia kifo kututawala. Lakini sasa neema ya Mungu inatawala juu ya dhambi na kifo kwa sababu ya wema wake wenye uaminifu. Na hii inatuletea maisha ya milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.


Matendo ya Mitume 6:1
Hivyo, je, mnadhani inatupasa tuendelee kutenda dhambi ili Mungu atupe neema nyingi zaidi na zaidi?


Matendo ya Mitume 6:14
Dhambi haitakuwa mtawala wenu, kwa sababu hamko chini ya sheria. Sasa mnaishi chini ya neema ya Mungu.


Matendo ya Mitume 6:15
Hivyo tufanye nini? Je, tutende dhambi kwa sababu tuko chini ya neema na siyo chini ya sheria? Hapana!


Matendo ya Mitume 11:5
Ndivyo ilivyo sasa. Mungu amewachagua watu wachache kwa neema yake.


Matendo ya Mitume 11:6
Na kama aliwachagua kwa neema yake, hivyo si kwa sababu ya matendo yao yaliyowafanya wawe watu wake. Kama wangefanywa kuwa watu wake kutokana na matendo yao, zawadi yake ya neema isingekuwa zawadi halisi.


Matendo ya Mitume 12:6
Sote tunazo karama tofauti tofauti. Kila karama ilikuja kwa sababu ya neema aliyotupa Mungu. Yule aliye na karama ya unabii anapaswa kuitumia karama hiyo kwa namna inayokubalika kiimani.


Matendo ya Mitume 16:20
Mungu mwenye kuleta amani atamwangamiza Shetani mapema na kuwapa nguvu juu yake. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi.


1 Wakorinto 1:3
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


1 Wakorinto 1:4
Ninamshukuru Mungu daima kwa sababu ya neema aliyowapa katika Kristo Yesu.


1 Wakorinto 15:10
Lakini, kwa sababu ya neema ya Mungu, ndivyo hivi nilivyo. Na neema aliyonipa haikupotea bure bila manufaa. Nilifanya kazi kwa bidii kuliko mitume wengine wote. (Lakini, kwa hakika si mimi niliyekuwa nafanya kazi. Ni neema ya Mungu iliyo ndani yangu.)


1 Wakorinto 16:23
Neema ya Bwana Yesu iwe pamoja nanyi.


2 Wakorinto 1:2
Neema na Amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.


2 Wakorinto 1:12
Hili ndilo tunalojivunia, na naweza kusema kwa dhamiri safi kwamba ni kweli: Katika kila kitu tulichofanya duniani, Mungu ametuwezesha kukifanya kwa moyo safi. Na hili ni kweli zaidi katika yale tuliyowatendea ninyi. Tulifanya hivyo kwa neema ya Mungu, si kwa hekima ambayo ulimwengu unayo.


2 Wakorinto 4:15
Mambo yote haya ni kwa ajili yenu. Na hivyo neema ya Mungu inatolewa kwa watu wengi zaidi na zaidi. Hili litaleta shukrani nyingi zaidi na utukufu kwa Mungu.


2 Wakorinto 6:1
Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu. Hivyo tunawasihi: Neema mliyoipokea kutoka kwa Mungu iwe na manufaa kwenu.


2 Wakorinto 8:1
Na sasa, kaka na Dada zetu, tunataka kuwaambia kile ambacho neema ya Mungu imefanya katika makanisa ya makedonia.


2 Wakorinto 8:9
Mnaifahamu neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mnafahamu kuwa aliacha utajiri wake mbinguni na kufanyika maskini kwa ajili yenu. Aliacha kila kitu ili ninyi mbarikiwe kwa wingi zaidi.


2 Wakorinto 9:14
Na wanapoomba kwa ajili yenu, watatamani wangekuwa pamoja nanyi. Watajisikia hivi kwa sababu ya neema ya ajabu aliyowapa Mungu.


2 Wakorinto 12:9
Lakini Bwana alisema, “Neema yangu ndiyo unayoihitaji. Ni pale tu unapokuwa dhaifu ndipo kila kitu kinapoweza kufanyika katika uwezo wangu.” Hivyo nitajivunia udhaifu wangu kwa furaha. Hapo ndipo uweza wa Kristo unaweza kukaa ndani yangu.


2 Wakorinto 13:13
Ninawaombea ili ninyi nyote mfurahie neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na Ushirika wa Roho Mtakatifu.


Wagalatia 1:3
Namwomba Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo awe mwema kwenu na awape neema na amani.


Wagalatia 1:6
Wakati mfupi tu uliopita Mungu aliwaita mkamfuata. Aliwaita katika neema yake kwa njia ya Kristo. Lakini sasa nashangazwa kwamba kwa haraka hivi mmegeuka mbali na kuamini kitu kingine tofauti kabisa na Habari Njema tuliyowahubiri.


Wagalatia 1:15
Lakini Mungu alikuwa na mpango maalumu kwa ajili yangu hata kabla sijazaliwa. Hivyo aliniita kwa neema yake. Na ilimpendeza


Wagalatia 2:21
Si mimi ninayeikataa neema ya Mungu kama vile haina manufaa yoyote. Kwa sababu ikiwa kwa kuifuata sheria ndivyo watu wanahesabiwa haki mbele za Mungu, basi Kristo alikufa pasipo faida!”


Wagalatia 5:4
Ikiwa utajaribu kufanyika mwenye haki mbele za Mungu kwa njia ya sheria, maisha yako na Kristo yamepotea, kwani umeiacha neema ya Mungu.


Wagalatia 6:18
Ndugu na dada zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.


Waefeso 1:2
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


Waefeso 1:6
Sifa kwake Mungu kwa sababu ya neema yake ya ajabu aliyotupa bure kupitia Kristo anayempenda.


Waefeso 1:7
Tumewekwa huru katika Kristo kupitia sadaka ya damu yake. Tumesamehewa dhambi kwa sababu ya wingi na ukuu wa neema ya Mungu.


Waefeso 1:8
Mungu alitupa bure neema hiyo yote, pamoja na hekima na uelewa wote,


Waefeso 2:5
Tulikuwa wafu kiroho kwa sababu ya matendo maovu tuliyotenda kinyume naye. Lakini yeye alitupa maisha mapya pamoja na Kristo. (Mmeokolewa na neema ya Mungu.)


Waefeso 2:7
Mungu alifanya hivi ili wema wake kwetu sisi tulio wa Kristo Yesu uweze kuonesha nyakati zote zijazo utajiri wa ajabu wa neema yake.


Waefeso 2:8
Nina maana ya kuwa mmeokolewa kwa neema kwa sababu mliweka imani yenu kwake. Hamkujiokoa ninyi wenyewe; bali ni zawadi kutoka kwa Mungu.


Waefeso 3:2
Mnajua hakika ya kuwa Mungu alinipa kazi hii kupitia neema yake ili niwasaidie.


Waefeso 3:7
Kwa kipawa cha neema ya Mungu, nilifanywa mtumishi wa kuihubiri Habari Njema. Alinipa neema hiyo kwa nguvu zake.


Waefeso 6:24
Naomba neema ya Mungu iwe pamoja nanyi nyote mnaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa pendo lisilo na mwisho.


Wafilipi 1:2
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Kristo Yesu, Bwana wetu, iwe pamoja nanyi.


Wafilipi 1:7
Ninajua niko sahihi kwa namna ile ninayowawazia ninyi nyote kwa sababu mko karibu sana na moyo wangu. Mmechangia sehemu muhimu sana katika neema ya Mungu kwa ajili yangu wakati huu nikiwa gerezani, na wakati wowote ninapoutetea na kuuthibitisha ukweli wa Habari njema.


Wafilipi 4:23
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na utu wenu wa ndani.


Wakolosai 1:2
Salamu kwenu kaka na dada zetu watakatifu na walio waaminifu katika Kristo mlioko Kolosai. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu ziwe pamoja nanyi.


Wakolosai 1:6
Habari Njema hii imezaa matunda na imeenea ulimwenguni kote. Na hicho ndicho kilichokuwa kikitokea tangu siku mliposikia kwa mara ya kwanza na kuelewa ukweli wa neema ya Mungu.


Wakolosai 4:18
Hii ni salamu yangu ambayo nimeiandika kwa mkono wangu mwenyewe: PAULO. Msiache kunikumbuka nikiwa hapa gerezani. Ninawaombea neema ya Mungu iwe pamoja nanyi nyote.


1 Wathesalonike 1:1
Salamu toka kwa Paulo, Sila, na Timotheo. Kwa kanisa lililoko Thesalonike lililo milki ya Mungu baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani ziwe zenu.


1 Wathesalonike 5:28
Neema ya Bwana wetu Yesu kristo iwe nanyi nyote.


2 Wathesalonike 1:2
Neema na amani viwe kwenu kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.


2 Wathesalonike 1:12
Kisha jina la Bwana wetu Yesu litaheshimiwa kwa sababu yenu, nanyi mtaheshimiwa kwa sababu yake, na mtaheshimiwa kwa sababu yake. Hii inaweza kutokea tu kwa neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.


2 Wathesalonike 2:16
Tunaomba kwamba Bwana Yesu Kristo na Mungu Baba yetu awafariji na kuwaimairisha katika kila jambo jema mnalotenda na kusema. Mungu alitupenda na kutupa kupitia neema matumaini ya ajabu na faraja isiyo na mwisho.


2 Wathesalonike 3:18
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.


1 Timotheo 1:2
Ninakuandikia wewe, Timotheo. Wewe ni kama mwanangu halisi kwa sababu ya imani yetu. Neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu ziwe pamoja nawe.


1 Timotheo 1:14
Lakini Bwana wetu alinipa kiwango kikubwa cha neema yake. Na pamoja na neema hiyo imani na upendo ulio katika Kristo Yesu vilifuata.


1 Timotheo 6:21
Watu wengine wanaodai kuwa na “elimu” wamepotea mbali kabisa kutokana na wanachoamini. Ninaomba neema ya Mungu iwe kwenu nyote.


2 Timotheo 1:2
Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa: Neema, rehema na amani iwe kwako kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.


2 Timotheo 1:9
Alituokoa na kutuita katika maisha ya utakatifu, sio kwa sababu ya kitu cho chote tulichokifanya wenyewe, bali kwa kusudi lake mwenyewe na neema, ambayo ametupa sisi kwa Kristo Yesu kabla ya mwanzo wa wakati,


2 Timotheo 2:1
Kwako wewe mwanangu, uwe hodari kwa njia ya neema inayopatikana kwa Kristo Yesu.


2 Timotheo 4:22
Bwana awe nawe. Neema ya Mungu iwe nanyi.


Tito 1:4
Nakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki: Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu iwe nanyi.


Tito 2:11
Maana Mungu ameidhihirisha neema yake inayookoa kwa watu wote.


Tito 3:7
Kwa neema yake Mungu alituweka huru mbali na dhambi. Akatufanya kuwa warithi wake tulio na tumaini la uzima wa milele.


Tito 3:15
Wote nilio pamoja nami wanakusalimu. Uwasalimu wote wanaotupenda katika imani. Neema ya Mungu iwe nanyi nyote.


Filemoni 1:3
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo ziwe pamoja nawe.


Filemoni 1:25
Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


Waebrania 2:9
Kwa kipindi kifupi Yesu aliwekwa chini kuliko malaika, lakini sasa tunamwona akiwa amevaa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa. Kwa sababu ya neema ya Mungu, Yesu alikufa kwa ajili ya kila mmoja.


Waebrania 4:16
Tukiwa na Yesu kama kuhani wetu mkuu, tunaweza kujisikia huru kuja mbele za kiti cha enzi cha Mungu ambako kuna neema. Hapo tunapata rehema na neema ya kutusaidia tunapokuwa tunahitaji.


Waebrania 10:29
Hivyo fikiri jinsi watu watakavyostahili kuhukumiwa zaidi ambao wanaonesha kumchukia mwana wa Mungu; watu wanaoonesha kuwa hawana heshima kwa sadaka ya damu iliyoanzisha agano jipya na mara moja ikawatakasa au wale wanaomkashifu Roho wa neema ya Mungu.


Waebrania 12:15
Muwe makini ili mtu asije akakosa kuipata neema ya Mungu. Muwe makini ili asiwepo atakayepoteza imani yake na kuwa kama gugu chungu linalomea miongoni mwenu. Mtu wa jinsi hiyo anaweza kuharibu kundi lenu lote.


Waebrania 13:9
Msiruhusu aina yoyote ya mafundisho mageni yawaongoze hadi katika njia isiyo sahihi. Itegemeeni neema ya Mungu pekee kwa ajili ya nguvu za kiroho, siyo katika sheria kuhusu vyakula. Kuzitii sheria hizi hakumsaidii yeyote.


Waebrania 13:25
Naomba neema ya Mungu iwe nanyi nyote.


Yakobo 4:6
Lakini Mungu ametuonesha sisi, rehema kuu zaidi. Ndiyo maana Maandiko yanasema: Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wale walio wanyenyekevu.


1 Petro 1:2
Kwa kadri ya mpango wa Mungu Baba alioufanya muda mrefu uliopita, mliteuliwa muwe wake kwa kufanywa watakatifu na Roho Mtakatifu. Mliteuliwa kuwa waatiifu kwa Mungu na kutakaswa na kujumuishwa miongoni mwa watu wa Agano Jipya kwa kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani ya Mungu viwe pamoja nanyi kwa wingi.


1 Petro 1:10
Manabii waliotabiri juu ya neema ambayo ingeoneshwa kwenu, walipeleleza kwa makini na kwa uangalifu wakaulizia habari za wokovu huu.


1 Petro 3:7
Vivyo hivyo, enyi waume inawapasa kuishi na wake zenu kwa kuelewa udhaifu alionao mwanamke na matumaini ya Mkristo. Hamna budi kuwapa heshima kwa sababu Mungu kwa sababu Mungu anawapa baraka zile zile anazowapa ninyi, yaani neema ya maisha ya kweli. Fanyeni hivi ili maombi yenu yasizuiliwe.


1 Petro 4:10
Mungu amewapa neema yake kwa namna nyingi mbalimbali. Hivyo muwe watumishi wema na kila mmoja wenu atumie kipawa chochote alichopewa kwa njia iliyo bora katika kuhudumiana ninyi kwa ninyi.


1 Petro 5:10
Ndiyo, mtateseka kwa muda mfupi. Lakini baada ya hapo, Mungu ataweka kila kitu sawa. Atawatia nguvu, atawasaidia na kuwashika msianguke. Yeye ni Mungu ndiye chanzo cha neema yote. Aliwachagua mshiriki katika utukufu wake ndani ya Kristo. Utukufu huo utadumu milele.


1 Petro 5:12
Sila ataileta barua hii kwenu. Nafahamu kwamba ni ndugu mwaminifu katika familia ya Mungu. Niliandika barua hii fupi kuwatia moyo na kuwaambia kuwa hii ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.


2 Petro 1:2
Mpewe neema na amani zaidi na zaidi, kwa sababu sasa mnamjua Mungu na Yesu Bwana wetu.


2 Petro 3:18
Lakini mkue katika neema na kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu ni wake, sasa na hata milele! Amina.


2 Yohane 1:3
Neema, rehema, na amani itakuwa pamoja nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa mwanaye, Yesu Kristo, kwa kadri tuishivyo katika kweli na upendo.


Yuda 1:4
Baadhi ya watu wamejiingiza kwa siri kwenye kundi lenu. Watu hawa wamekwisha kuhukumiwa kuwa wakosaji kwa sababu ya matendo yao. Zamani zilizopita manabii waliandika kuhusu watu hao. Wako kinyume na Mungu. Wameigeuza neema ya Mungu kujihalalishia kutenda chochote wanachotaka. Wanakataa kumtii Mkuu aliye peke yake, Bwana wetu Yesu Kristo.


Ufunuo wa Yohane 1:4
Kutoka kwa Yohana, Kwenda kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema na amani ziwe kwenu kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo daima na anayekuja; na kutoka katika roho saba zilizoko mbele ya kiti chake cha enzi;


Ufunuo wa Yohane 22:21
Neema ya Bwana Yesu iwe pamoja na watu wote.


Swahili Bible (TKU) 2017
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi Toleo la Awali © 2017 Bible League International