A A A A A


Tafuta

Yohane 12:36
Hivyo wekeni matumaini yenu katika nuru wakati bado mkiwa nayo. Jinsi hiyo mtakuwa watoto wa nuru.” Yesu alipomaliza kusema mambo hayo, aliondoka na kwenda mahali ambapo watu wasingeweza kumwona.


Waroma 27:20
Kwa siku nyingi hatukuweza kuliona jua au nyota. Dhoruba ilikuwa mbaya sana. Tulipoteza matumaini yote ya kuendelea kuwa hai, tulidhani tutakufa.


Waroma 27:31
Lakini Paulo alimwambia ofisa wa jeshi na askari wengine, “Iwapo watu hawa hawatakaa ndani ya meli, mtapoteza matumaini yote ya kupona.”


Matendo ya Mitume 15:4
Chochote kilichoandikwa zamani kiliandikwa ili kitufundishe sisi. Maandiko haya yaliandikwa ili yatupe matumaini yanayokuja kwa njia ya subira na kutia moyo kunakoletwa nayo.


Matendo ya Mitume 15:12
Na Isaya anasema, “Mtu mmoja atakuja kutoka katika ukoo wa Yese. Atainuka na kutawala juu ya mataifa, na wataweka matumaini yao kwake.”


Matendo ya Mitume 15:13
Naomba kwamba Mungu aletaye matumaini awajaze furaha na amani kadri mnavyomwamini yeye. Na hii isababishe tumaini lenu liongezeke hadi lifurike kabisa ndani yenu kwa nguvu za Roho Mtakatifu.


2 Wakorinto 1:13
Tunawaandikia mambo mnayoweza kusoma na kuyaelewa. Na nina matumaini kuwa mtayaelewa inavyopasa


2 Wakorinto 13:6
Lakini ni matumaini yangu kuwa mtagundua ya kwamba hatujashindwa jaribio hilo.


Wagalatia 5:5
Ninasema hivi kwa sababu tumaini letu la kufanywa wenye haki mbele za Mungu huja kwa imani. Na kwa nguvu ya Roho kwa njia ya imani, tunangoja kwa utulivu na kwa matumaini yenye ujasiri hukumu ya Mungu inayotuweka huru.


Waefeso 6:10
Hapa lipo neno moja la mwisho la ushauri: Mtegemeeni Bwana kwa ajili ya nguvu zenu. Wekeni matumaini yenu katika nguvu zake kuu.


Wafilipi 3:11
Kisha mimi mwenyewe naweza kuwa na matumaini kwamba nitafufuliwa kutoka kwa wafu.


1 Wathesalonike 4:13
Kaka na dada, tunawataka mfahamu habari za wale waliokufa. Hatupendi muwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini.


2 Wathesalonike 2:16
Tunaomba kwamba Bwana Yesu Kristo na Mungu Baba yetu awafariji na kuwaimairisha katika kila jambo jema mnalotenda na kusema. Mungu alitupenda na kutupa kupitia neema matumaini ya ajabu na faraja isiyo na mwisho.


1 Timotheo 4:10
Tunayo matumaini kwa Mungu aliye hai, Mwokozi wa watu wote. Ambaye hasa, ni Mwokozi wa wale wote wanaomuamini. Na hii ndiyo sababu tunafanya kazi na kupambana.


Filemoni 1:22
Pamoja na hayo naomba uniandalie chumba cha kufikia, kwa sababu nina matumaini kwamba kwa maombi yenu nitaachiliwa na kuletwa kwenu.


1 Petro 1:13
Hivyo mkeshe katika fahamu zenu na kuwa na kiasi. Yawekeni kikamilifu matumaini yenu katika baraka mtakazopewa wakati Yesu Kristo atakapofunuliwa.


1 Petro 1:21
Kupitia Kristo mmekuwa waamini katika Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na kumpatia utukufu. Ili imani yenu na matumaini yawekwe katika Mungu.


1 Petro 3:7
Vivyo hivyo, enyi waume inawapasa kuishi na wake zenu kwa kuelewa udhaifu alionao mwanamke na matumaini ya Mkristo. Hamna budi kuwapa heshima kwa sababu Mungu kwa sababu Mungu anawapa baraka zile zile anazowapa ninyi, yaani neema ya maisha ya kweli. Fanyeni hivi ili maombi yenu yasizuiliwe.


1 Yohane 3:3
Ni mtakatifu, na kila aliye na matumaini haya katika yeye huendelea kuwa mtakatifu.


Swahili Bible (TKU) 2017
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi Toleo la Awali © 2017 Bible League International