A A A A A


Tafuta

Marko 1:11
Sauti ikasikika toka mbinguni, “Wewe ni mwanangu, ninayekupenda, napendezwa nawe sana.”


Luka 3:22
na Roho Mtakatifu aliyekuwa katika umbo la njiwa akashuka juu yake. Sauti ikasikika toka mbinguni, “Wewe ni mwanangu, ninayekupenda, napendezwa nawe sana.”


Yohane 13:34
“Nawapa amri mpya: Pendaneni ninyi kwa ninyi. Mnapaswa kupendana kama mimi nilivyowapenda ninyi.


Yohane 21:15
Walipomaliza kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda kuliko watu wote hawa wanavyonipenda?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, unajua kuwa nakupenda.” Kisha Yesu akamwambia, “Wachunge wanakondoo wangu.”


Yohane 21:16
Kwa mara nyingine Yesu akamwambia, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, wewe unajua kuwa nakupenda.” Kisha Yesu akasema, “Watunze kondoo wangu.”


Yohane 21:17
Mara ya tatu Yesu akasema, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika kwa sababu Yesu alimuuliza mara tatu, “Unanipenda?” Akasema, “Bwana, unafahamu kila kitu. Unajua kuwa nakupenda!” Yesu akamwambia, “Walinde kondoo wangu.


Matendo ya Mitume 13:10
Upendo hauwaumizi wengine. Hivyo kupenda ni sawa na kuitii sheria yote.


1 Wathesalonike 3:12
Tunaomba kuwa Bwana ataufanya upendo wenu uendelee kukua. Tunaomba kuwa atawapa kupendana zaidi na zaidi miongoni mwenu na kwa watu wote. Tunaomba kuwa mtampenda kila mmoja kwa namna ile ile ambayo sisi tuliwapenda ninyi.


1 Wathesalonike 4:9
Hatuna haja ya kuwaandikia juu ya kuwa na upendo kwa katika Kristo. Mungu amekwisha kuwafundisha kupendana ninyi kwa ninyi.


1 Timotheo 6:4
Wanajivunia wanayoyafahamu, lakini hawaelewi chochote. Wamepagawa na wana ugonjwa wa kupenda mabishano na mapigano ya maneno. Na hayo yanaleta wivu, ugomvi, matusi, na uovu wa kutoaminiana.


1 Timotheo 6:10
Kupenda fedha kunasababisha aina zote za uovu. Watu wengine wamegeuka kutoka kwenye imani yetu kwa sababu wanataka kupata fedha nyingi zaidi. Lakini wamejisababishia wenyewe maumivu mengi na huzuni.


2 Timotheo 3:2
Watu watajipenda wenyewe na kupenda fedha. Watakuwa na majivuno na wenye jeuri. Watawatukana wengine kwa matusi. Hawatawatii wazazi wao. Watakuwa wasio na shukrani. Watapinga kila kinachompendeza Mungu.


Waebrania 13:1
Endeleeni kupendana ninyi kwa ninyi kama kaka na dada katika Kristo.


Waebrania 13:5
Yatunzeni maisha yenu yawe huru kutokana na kupenda fedha. Na mridhike na kile mlichonacho. Mungu amesema: “Sitakuacha kamwe; Sitakukimbia kamwe.”


1 Petro 1:22
Sasa kwa vile mmejitakasa wenyewe kwa kuitii kweli hadi mwisho kwamba mtaonesha upendo wa kweli wa kindugu, jitahidini kupendana ninyi kwa ninyi kwa mioyo iliyo safi.


1 Petro 5:2
mlitunze kundi la watu mnalowajibika kwalo. Ni kundi lake Mungu. Basi lichungeni kwa moyo wa kupenda na si kwa kulazimishwa. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka. Fanyeni hivyo kwa sababu mnafurahi kutumika, na si kwa sababu mnataka pesa.


2 Yohane 1:6
Na hii ndiyo maana ya kupenda: kuishi kulingana na amri zake. Na amri ya Mungu ni hii: Kwamba muishi maisha ya upendo. Mliisikia amri hii toka mwanzo.


Ufunuo wa Yohane 3:9
Sikiliza! Kuna kundi la Shetani. Wanasema kuwa wao ni Wayahudi, lakini ni waongo. Si Wayahudi halisi. Nitawafanya waje mbele yako na kusujudu kwenye miguu yako. Watajua ya kuwa ninakupenda.


Swahili Bible (TKU) 2017
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi Toleo la Awali © 2017 Bible League International