1 |
Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Luko Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa na Sauli. |
2 |
Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.” |
3 |
Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao. |
4 |
Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro. |
5 |
Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao. |
6 |
Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar Yesu. |
7 |
Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa, Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. |
8 |
Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. |
9 |
Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule Elima mchawi, |
10 |
kamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka? |
11 |
Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.” Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huko na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. |
12 |
Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana. |
13 |
Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perge huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko akarejea Yerusalemu. |
14 |
Kutoka Perge wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi wakaketi. |
15 |
Baada ya kusomwa Torati na vitabu vya manabii, viongozi wa lile sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwasaidia watu hawa, tafadhali lisemeni.” |
16 |
Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu. |
17 |
Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile. |
18 |
Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani. |
19 |
Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao. |
20 |
Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli. |
21 |
Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. |
22 |
Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Ambaye pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’ |
23 |
“Kutoka katika uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi. |
24 |
Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli. |
25 |
Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’ |
26 |
“Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu. |
27 |
Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye. |
28 |
Ijapokuwa hawakupata sababu yo yote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe. |
29 |
Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini. |
30 |
Lakini Mungu alimfufua kutoka katika wafu. |
31 |
Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu. |
32 |
“Nasi tunawaletea habari njema kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu |
33 |
sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: “ ‘Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.’ |
34 |
Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika nilizomwahidi Daudi.’ |
35 |
Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi, “ ‘Hutamwacha Mtakatifu wako aone uharibifu.’ |
36 |
“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. |
37 |
Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu. |
38 |
“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. |
39 |
Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. |
40 |
Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate: |
41 |
“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, mkastaajabu, mkaangamie, kwa maana nitatenda jambo wakati wenu ambalo hamtasadiki, hata kama mtu akiwaambia.’ ” |
42 |
Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato nyingine inayofuata. |
43 |
Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. |
44 |
Sabato iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la Mungu. |
45 |
Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu na kunena maneno ya kashfa kuhusu yale Paulo aliyokuwa akisema. |
46 |
Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu Mataifa. |
47 |
Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru: “ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu Mataifa, ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’ ” |
48 |
Watu Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. |
49 |
Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. |
50 |
Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka kwenye eneo lao. |
51 |
Hivyo Paulo na Barnaba wakakung'uta mavumbi kutoka kwenye miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio. |
52 |
Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.
|
Swahili Bible 2015 Contemporary |
Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Waroma 13:1 |
Waroma 13:2 |
Waroma 13:3 |
Waroma 13:4 |
Waroma 13:5 |
Waroma 13:6 |
Waroma 13:7 |
Waroma 13:8 |
Waroma 13:9 |
Waroma 13:10 |
Waroma 13:11 |
Waroma 13:12 |
Waroma 13:13 |
Waroma 13:14 |
Waroma 13:15 |
Waroma 13:16 |
Waroma 13:17 |
Waroma 13:18 |
Waroma 13:19 |
Waroma 13:20 |
Waroma 13:21 |
Waroma 13:22 |
Waroma 13:23 |
Waroma 13:24 |
Waroma 13:25 |
Waroma 13:26 |
Waroma 13:27 |
Waroma 13:28 |
Waroma 13:29 |
Waroma 13:30 |
Waroma 13:31 |
Waroma 13:32 |
Waroma 13:33 |
Waroma 13:34 |
Waroma 13:35 |
Waroma 13:36 |
Waroma 13:37 |
Waroma 13:38 |
Waroma 13:39 |
Waroma 13:40 |
Waroma 13:41 |
Waroma 13:42 |
Waroma 13:43 |
Waroma 13:44 |
Waroma 13:45 |
Waroma 13:46 |
Waroma 13:47 |
Waroma 13:48 |
Waroma 13:49 |
Waroma 13:50 |
Waroma 13:51 |
Waroma 13:52 |
|
|
|
|
|
|
Waroma 1 / War 1 |
Waroma 2 / War 2 |
Waroma 3 / War 3 |
Waroma 4 / War 4 |
Waroma 5 / War 5 |
Waroma 6 / War 6 |
Waroma 7 / War 7 |
Waroma 8 / War 8 |
Waroma 9 / War 9 |
Waroma 10 / War 10 |
Waroma 11 / War 11 |
Waroma 12 / War 12 |
Waroma 13 / War 13 |
Waroma 14 / War 14 |
Waroma 15 / War 15 |
Waroma 16 / War 16 |
Waroma 17 / War 17 |
Waroma 18 / War 18 |
Waroma 19 / War 19 |
Waroma 20 / War 20 |
Waroma 21 / War 21 |
Waroma 22 / War 22 |
Waroma 23 / War 23 |
Waroma 24 / War 24 |
Waroma 25 / War 25 |
Waroma 26 / War 26 |
Waroma 27 / War 27 |
Waroma 28 / War 28 |