೧ |
Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba. |
೨ |
Daudi akajua ya kwamba Bwana amemweka imara ili amiliki juu ya Israeli, kwa kuwa milki yake imeinuka kwa ajili ya watu wake Israeli. |
೩ |
Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti. |
೪ |
Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani; |
೫ |
na Ibhari, na Elishua, na Elpeleti; |
೬ |
na Noga, na Nefegi, na Yafia; |
೭ |
na Elishama, na Eliada, na Elifeleti. |
೮ |
Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao. |
೯ |
Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai. |
೧೦ |
Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye Bwana akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako. |
೧೧ |
Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu. |
೧೨ |
Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto. |
೧೩ |
Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni. |
೧೪ |
Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; uwageukie mbali, ukawajie huko kuielekea miforsadi. |
೧೫ |
Kisha itakuwa utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo utakapokwenda nje vitani; kwa maana ndipo Mungu ametoka mbele yako, awapige jeshi la Wafilisti. |
೧೬ |
Daudi akafanya kama vile Mungu alivyomwamuru; wakawapiga jeshi la Wafilisti toka Geba mpaka Gezeri. |
೧೭ |
Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye Bwana akawaletea mataifa yote hofu yake.
|
Kannada Bible (KNCL) 2016 |
No Data |