A A A A A
Facebook Instagram Twitter
Kiswahili Biblia 2015 Contemporary

Proverbis 31
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
2
kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio.
3
Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.
4
Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu.
5
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6
katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.
7
Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe, mche BWANA ukajiepushe na uovu.
8
Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako.
9
Mheshimu BWANA kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote;
10
ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
11
Mwanangu, usidharau marudi ya BWANA na usichukie kukaripiwa naye,
12
kwa sababu BWANA huwarudi wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.
13
Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu,
14
kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
15
Hekima ana thamani kuliko marijani, hakuna cho chote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye.
16
Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume, katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima.
17
Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani.
18
Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa.
19
Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;
20
kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande.
21
Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako;
22
ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako.
23
Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa;
24
ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.
25
Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu,
26
kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
27
Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda.
28
Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho,” wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.
29
Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.
30
Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lo lote.
31
Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote,
32
kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
33
Laana ya BWANA i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.
34
Huwadhihaki wale wanaodhihaki kwa kiburi lakini huwapa neema wanyenyekevu.
35
Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.Proverbis 3:1

Proverbis 3:2

Proverbis 3:3

Proverbis 3:4

Proverbis 3:5

Proverbis 3:6

Proverbis 3:7

Proverbis 3:8

Proverbis 3:9

Proverbis 3:10

Proverbis 3:11

Proverbis 3:12

Proverbis 3:13

Proverbis 3:14

Proverbis 3:15

Proverbis 3:16

Proverbis 3:17

Proverbis 3:18

Proverbis 3:19

Proverbis 3:20

Proverbis 3:21

Proverbis 3:22

Proverbis 3:23

Proverbis 3:24

Proverbis 3:25

Proverbis 3:26

Proverbis 3:27

Proverbis 3:28

Proverbis 3:29

Proverbis 3:30

Proverbis 3:31

Proverbis 3:32

Proverbis 3:33

Proverbis 3:34

Proverbis 3:35Proverbis 1 / Pro 1

Proverbis 2 / Pro 2

Proverbis 3 / Pro 3

Proverbis 4 / Pro 4

Proverbis 5 / Pro 5

Proverbis 6 / Pro 6

Proverbis 7 / Pro 7

Proverbis 8 / Pro 8

Proverbis 9 / Pro 9

Proverbis 10 / Pro 10

Proverbis 11 / Pro 11

Proverbis 12 / Pro 12

Proverbis 13 / Pro 13

Proverbis 14 / Pro 14

Proverbis 15 / Pro 15

Proverbis 16 / Pro 16

Proverbis 17 / Pro 17

Proverbis 18 / Pro 18

Proverbis 19 / Pro 19

Proverbis 20 / Pro 20

Proverbis 21 / Pro 21

Proverbis 22 / Pro 22

Proverbis 23 / Pro 23

Proverbis 24 / Pro 24

Proverbis 25 / Pro 25

Proverbis 26 / Pro 26

Proverbis 27 / Pro 27

Proverbis 28 / Pro 28

Proverbis 29 / Pro 29

Proverbis 30 / Pro 30

Proverbis 31 / Pro 31