A A A A A
Matthayo 1
1
Hii ni historia ya ukoo wa Yesu, Masihi. Alitoka katika ukoo wa Daudi, aliyetoka katika ukoo wa Ibrahimu.
2
Ibrahimu alikuwa baba yake Isaka. Isaka alikuwa baba yake Yakobo. Yakobo alikuwa baba wa Yuda na ndugu zake.
3
Yuda alikuwa baba wa Peresi na Zera. (Mama yao alikuwa Tamari.) Peresi alikuwa baba yake Hezroni. Hezroni alikuwa baba yake Ramu.
Kiswahili Biblia (TKU) 2017

1
Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:
2
Abrahamu akamzaa Isaki, Isaki akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake,
3
Yuda akamzaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Aramu,
Kiswahili Biblia 2015 Contemporary

1
Yesu Kristo alikuwa wa ukoo wa Daudi, wa ukoo wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake:
2
Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake,
3
Yuda alimzaa Peresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Peresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
Kiswahili Biblia (BHN) 2001

1
Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2
Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3
Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
Kiswahili Biblia 1997

1
Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake:
2
Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake,
3
Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
Kiswahili Biblia 1850